Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Burkina Faso: Macron amuomba Traoré kutoa 'ufafanuzi'

Rais wa Ufaransa amemtaka mwenzake wa Burkina Faso kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na habari iliyotolewa na shirika la habari nchini Burkina Faso kwamba serikali ya Ouagadougou imeomba wanajeshi wa Ufaransa kuondoka kwenye ardhi yake ndani ya mwezi mmoja;

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari pamoja na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Jumapili hii, Januari 22, 2023 kwenye Ikulu ya Élysée mjini Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari pamoja na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Jumapili hii, Januari 22, 2023 kwenye Ikulu ya Élysée mjini Paris. AP - Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

"Nasubiri rais wa mpito Ibrahim Traoré aweze kuzungumza. Maoni ya rais wa Ufaransa, kufuatia ombi kutoka serikali ya kijeshi ya Burkina Faso ya kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Burkina Faso. 

Siku ya Jumamosi jioni, Shirika la Habari la Burkinabe (AIB) lilidai kuwa serikali ya Burkina Faso "imechukua hatua" ya kutaka kuondoka kwa jeshi la Ufaransa "kwenye ardhi yake", ndani ya mwezi mmoja. Haya yanajiri wakati maandamano ya raia dhidi ya uwepo wa jeshi la Ufaransa yameongezeka.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alijibu matangazo ya Shirika la Habari la Burkina Faso kutoka Paris, wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa kwa hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya mkataba wa maridhiano kati ya Ufaransa na Ujerumani.

Kulingana na AIB, Burkina Faso "imepitisha uamuzi wa kuondoka kwa jeshi la Ufaransa kwenye ardhi yake". Shirika hilo la habari linashikilia kuwa serikali ilishutumu, wiki iliyopita, makubaliano ambayo yaliyofikiwa tangu 2018 kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.

Wanajeshi 400 wa kikosi maalum cha Operesheni Saber wana mwezi mmoja wa kuondoka nchini Burkina faso. Lakini  Emmanuel Macron anasema, tangazo hili linahitaji ufafanuzi zaidi kutoka kwa Kapteni Ibrahim Traoré, rais wa mpito wa Burkina Faso.

Ninasubiri rais wa mpito Traoré aweze kuzungumza, kwa sababu nilielewa kwamba jumbe ambazo zilikuwa zimetoka katika hatua hii zilikuwa sehemu ya mkanganyiko mkubwa, wakati rais mwenyewe alikuwa ziarani nje ya mji mkuu. Kwa hivyo nadhani tunapaswa kuwa waangalifuzaidi, na kuangalia kile ambacho ni maalum kwa baadhi ya watu katika eneo hili, ambao wanaweza kuwa na uhusiano na kile tunachopitia huko Ukraine, ikiwa ni pamoja na kile ambacho marafiki zetu wa Urusi wanaweza kutumia kama uongo. Tunasubiri ufafanuzi kutoka kwa Bw. Traoré kuhusu suala hili.

Tangu mapinduzi ya kijeshi mwezi Septemba mwaka uliyopita, maandamano dhidi ya uwepo wa jeshi la Ufaransa yameongezeka huko Ouagadougou. Mwanzoni mwa mwezi Januari, mamlaka ya mpito iliomba kuondoka kwa balozi wa Ufaransa nchini Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.