Pata taarifa kuu
SOMALIA- USALAMA

Wapiganaji 30 wa al-Shabab wamewaua katika Shambulio la anga la Marekani

Wanajeshi wa Marekani kwa ushirkiano na wale wa Somalia, wametekeleza shambulio la angani ambalo limewaua wapiganaji 30 wa Kiislamu wa al-Shabab,imesema ripoti ya  jeshi la Marekani.

Wapiganaji wa al-Shabab
Wapiganaji wa al-Shabab AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo imefanyika  karibu na mji wa Galcad, kilomita 260 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Mogadishu.

Wanajeshi wa serikali ya Mogadishu wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa al-Shabab katika kipindi cha siku chache zilizopita kuudhibiti mji huo.

Shambulio hili linajiri siku chache baada ya Hapo awali wanamgambo hao kuawaua wanajeshi saba wa serikali  baada ya kuvamia kambi ya kijeshi huko Galcad.

Licha ya shambulio katika kambi ya jeshi, wizara ya habari ya Somalia ilisema makumi ya wanamgambo hao waliuawa.

Al-Shabab imekuwa ikipambana na serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2006, kwa lengo la kulazimisha utawala wa Kiislamu wenye itikadi kali nchini humo.

Jumatatu iliyopita serikali ilisema jeshi lake na wanamgambo wa ndani wameuteka mji wa bandari wa Harardhere, ambao umekuwa kituo kikuu cha usambazaji cha al-Shabab tangu 2010.

Katika ripoti yake kuhusu kundi la Galcad linalopigana na Kamandi ya Marekani ya Afrika ilisema magari matatu ya al-Shabab yaliharibiwa na "kamandi hiyo inatathmini kuwa hakuna raia aliyejeruhiwa au kuuawa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.