Pata taarifa kuu
DRC

Aliyekuwa msaidizi wa rais Tshisekedi apelekwa gerezani

Nchini DRC, Fortunat Biselele, aliyekuwa msaidizi wa rais Felix Tshisekedi, amepelekwa katika Gereza Kuu la Makala jijini Kinshasa, baada ya saa sita na viongozi wa mashtaka.

Fortunat Biselele, aliyekuwa msaidizi wa rais Felix Tshisekedi, akipelekwa katika Gereza Kuu la Makala jijini Kinshasa, Januari 20 2023
Fortunat Biselele, aliyekuwa msaidizi wa rais Felix Tshisekedi, akipelekwa katika Gereza Kuu la Makala jijini Kinshasa, Januari 20 2023 © Pascal Mulegwa / RFI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema, Biselele, aliyekuwa binafsi wa rais Tshisekedi, alipelekwa katika Gereza hilo Ijumaa usiku.

Mikanda miwili ya vídeo, imeonekana, ikimwonesha Biselele, akisindikizwa wanajeshi, kwenda katika Ofisi ya kiongozi wa mashtaka.

Baadaye usiku, alionekana akiwa anasindikzwa na polisi kwenda Gerezani.

Biselele, aliondolewa kwenye Baraza la Mawaziri Januari 14, na kuzuiwa , lakini mpaka sasa hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kukamatwa na kusimamishwa kwake kazi.

Hata hivyo, ripoti kutoka kwenye jarida la Africa Intelligence,inaeleza mshauri huyo wa zamani wa rais Tshisekedi, alikuwa anashukiwa kushirikiana na serikali ya rais Paul Kagame nchini Rwanda.

Inaripotiwa kuwa, mwanzano mwa utawala wa rais Tshisekedi, alijaribu kumleta karibu na rais Kagame.

Uhusiano kati ya Kigali na Kinshasa, umeyumba, kufuatia madai ya DRC kuwa Rwanda, inawaunga mkono waasi wa M 23, shutuma ambazo rais Kagame, ameendelea kukanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.