Human Rights Watch yadai Rwanda inakiuka haki ya kujieleza
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, linaishtumu Rwanda kwa kukiuka haki ya kujieleza na inataka kurekebisha sheria yake.
Imechapishwa:
Cheza - 00:31
Hii inakuja baada kufungwa jela kwa mpinzani wa serikali ya Kigali, Théophile Ntirutwa kutoka chama cha Dalfa-Umurinzi, aliyekamatwa mwaka 2010 kwa madai ya kusambaza tarifa za uongo, zilizolenga kuichafua nchi hiyo.
Lewis Mudge, ni Mkurugenzi Mkuu wa Human Rights Watch barani Afrika.
“Imekuwa ni vigumu kwa mtu yeyote kuikosea serikali ya Rwanda.”ameeleza Lewis Mudge.
Taarifa ya HRW inakuja wakati huu baadhi wanasiasa wa upinzani katika baadhi ya mataifa ya Afrika wakizituhumu serikali zilizo madarakani kwa kuwahanagisha.