Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI- SIASA

Sudan Kusini: UN imetoa wito wa maandalizi ya mapema ya uchaguzi

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Nicholas Haysom, anaitaka serikali ya Juba kuanza maandalizi ya mapema, ili kufanikisha uchaguzi mkuu, uliopangwa kufanyika mwaka ujao.Mwandishi wetu James Shimanyula, anaeleza zaidi

 Salva Kiir, Rais wa Sudan Kusini
Salva Kiir, Rais wa Sudan Kusini AFP - PETER LOUIS GUME
Matangazo ya kibiashara

Hii hapa kauli ya haraka ambayo Haysom alitoa kwa Rais Salva Kiir na ambayo anafaa kutekeleza haraka kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.

"Mipango ya uchaguzi wa mwaka ujao inafaa kufanywa mwaka huu wa elfu-mbili-ishirini-na-tatu na wala si mwaka ujao na yale ambayo hayajatekelezwa yanafaa kutekelezwa haraka.  Wasiwasi nilio nayo ni kwamba ukosefu wa mipango ya haraka ya uchaguzi utachelewesha uchaguzi." amesema Nicholas Haysom.

Akigusia swala la mapigano ya kikabila ambayo yameikumba mikoa miwili mikubwa iliyoko kaskazini mashariki mwa jiji kuu Juba, Haysom alisema:

"Mapigano yanayoendelea  ambayo yanatokana na misingi ya kikabila na uharibifu. Yanarudisha nyuma maendeleo yaliyopo na hata yanaweza kusambaratisha mipango ya kuleta amani ya kudumu. Mapigano haya yanazidisha joto la chuki na mgawanyiko." amesisitiza Nicholas Haysom.

Akijibu matamshi yaliyotolewa na Haysom, waziri wa habari wa Sudan Kusini, Michael Makwei alisema:

"Tuna hakika kuwa tutafanya uchaguzi mwaka ujao. Tutakamilisha  utayarishaji wa katiba mpya. Tayari tumeweka saini kwenye kipengele kinachohusiana na uandalizi wa katiba mpya. Tumeweka saini  sharia za uchaguzi. Tuko tayari kuzima mapigano yanayoendelea.  Nini tena? Mapigano ya kikabila kamwe hayawezi kusimamisha kufanyika kwa uchaguzi." ameeleza Michael Makwei.

Tangu Sudan Kusini itangazwe nchi huru julai tisa mwaka 2011 imekumbwa na mtiririko wa mapigano ya mara kwa mara ya kikabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.