DR Congo : Watu 10 wameuawa katika shambulio la bomu kanisani
Watu 10 wameripotiwa kuuawa wakiwemo watoto na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa, baada ya kutekelezwa shambulio la bomu kwenye kanisa moja mjini Kasindi katika mpaka wa DRC na Uganda, kilometa 80 kaskazini mwa mji wa Beni.
Imechapishwa:
Cheza - 00:23
Waasi wa ADF wenye uhusiani na mtandao wa Al Qaeda wakitajwa kuhusika.
Luteni Mopero Momitabonge, ni kamanda wa polisi kwenye mji wa Kasindi.
“Watu wameumia wengi, wengine wako hosipitalini zaidi ya kumi na wawili.” amesema Mopero Momitabonge
Shambulio hili limetekelezwa licha ya operesheni za pamoja za kijeshi zinazoendelea kwenye eneo hilo dhidi ya waasi hao kati ya jeshi la serikali FARDC na lile la Uganda, UPDF.