Pata taarifa kuu

Ukraine: Ufaransa na Ujerumani zaitaka Afrika kulaani Urusi

Wakuu wa diplomasia ya Ufaransa na Ujerumani siku ya Ijumaa wametoa wito kwa nchi za Afrika kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku wakisisitiza juu ya nia ya Umoja wa Ulaya, EU, ya kuzidisha uhusiano wake na Umoja wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock (kushoto) na mwenzake wa Ufaransa Catherine Colonna (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Adama, Ethiopia, Januari 12, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock (kushoto) na mwenzake wa Ufaransa Catherine Colonna (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Adama, Ethiopia, Januari 12, 2023. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

"Ni muhimu (kuhusu vita vya Ukraine) kukumbuka kwamba kuna mchokozi na kushambuliwa na ni muhimu kila mtu amwambie mchokozi kwamba lazima aache uchokozi wake," amesema Waziri wa Ufaransa Catherine Colonna mjini Addis Ababa.

"Tuna maslahi ya pamoja na tuna matarajio ya marafiki zetu wa Afrika na tumeshiriki nanyi," ameongeza, baada ya mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja huo.

Ujumbe kama huo umeotolewa na mwenzake wa Ujerumani Annalena Baerbock: "Amani barani Ulaya inashambuliwa, tunawahitaji, tunahitaji Afrika kulinda amani".

Mwezi Machi mataifa kadhaa ya Afrika yalijizuia, wakati wa kura ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu azimio la kutaka 'Urusi iache mara moja kutumia nguvu dhidi ya Ukraine'.

"Tunaona athari za vita hivi vya kikatili vya Urusi kote ulimwenguni na hasa katika Pembe ya Afrika," ambapo Urusi inatumia nafaka kama silaha ya vita kwa kuzuia usafirishaji wa Ukraine, Baerbock ameongeza.

Mawaziri hao wawili waliowasili nchini Ethiopia siku ya Alhamisi kwa ziara ya siku mbili, wamezungumza pamoja na Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

"Tunataka kuimarisha uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika," amesema Bi Baerbock, ambaye amekumbusha uungaji mkono wa Ujerumani wa mageuzi ya Baraza la Usalama la Kudumu la Umoja wa Mataifa, ambayo yatawezesha bara la Afrika kuwa na viti viwili vya kudumu.

Bi. Colonna pia ametetea "ushirikiano bora wa bara la Afrika katika utawala wa kimataifa" na uwakilishi bora wa bara hilo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nafasi ya Umoja wa Afrika ndani ya kundi la nchi 20 zilizostawi kiviwanda (G20).

Akielezea kutokuwepo kwa Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama "ukosefu wa haki ambao lazima urekebishwe", Moussa Faki Mahamat amekaribisha "uungaji mkono" wa Ufaransa na Ujerumani. Marekani pia inaunga mkono mageuzi hayo.

Baada ya mkutano, karibu mwaka mmoja uliopita, kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, "tunataka kuendelea kujenga juu ya kanuni ambazo ziliidhinishwa" ili kuimarisha ushirikiano kati ya washirika hao wawili, amebainisha Bi Colonna.

"Tulikuwa na ugumu wa kuandaa faili, kwa sababu mara nyingi wanawake hawa hawana utambulisho wa kweli wa baba wa watoto wao", anabainisha. Vipimo vya DNA kwa hivyo haziwezekani au ni ngumu sana kufanya. "Lakini tulikusanya shuhuda, kutoka kwa wasaidizi, kutoka kwa machifu wa kijiji...", anaongeza "Maman Zawadi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.