Pata taarifa kuu
RWANDA-MAHAKAMA-HAKI

Njia mbadala ya kupunguza mrundikanano wa kesi mahakamani Rwanda

Katika mkakati wake wa kujaribu kupunguza kesi zinazorundikana mahakamani, Serikali ya Rwanda, wiki hii imezindua sera mpya zinazolenga kuendeleza mfumo mbadala wa utoaji haki, ikilenga kuhamasisha majadiliano katika kutatua baadhi ya migogoro na majaji kuwa na uwezo wa kutoa hukumu ambazo hazilazimu mtu kwenda jela.

Rais wa  Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Anastase Nabahire, ni mkurugenzi wa ofisi ya kuratibu utoaji haki nchini

“Limezungumziwa swala la kuachiwa huru kwa marsharti pia mipangilio kwa faida ya kila mtu hivyo tunajifunza namna ya kuweka mfumo wa bangili za kieletroniki.”Amesema Anastase Nabahire.

Swala la mirundiko ya kesi kwenye mahakama limekuwa likishuhudiwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Mamlaka zikija na njia mbadala ya kutatua changamoto hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.