Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- MAZUNGUMZO - AMANI

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani na Ufaransa wanazuru Ethiopia

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Ujerumani na Ufaransa wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, jijini Addis Ababa kuhusu amani ya eneo la jimbo la Tigray.

Catherine Colonna, Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa
Catherine Colonna, Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa AP - Jacquelyn Martin
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Ahmed, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameandika kuwa amekutana na Mawaziri hao, Catherine Collonna, kutoka Ufaransa na Annalena Baerbock, kutoka Ujerumani, kujadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la usalama, mazungumzo ambayo amesema yamekuwa yenye mafanikio.

Baada ya kuwasili jijini Addis Ababa, Mawaziri hao walisema, walikuja nchini humo kuunga mkono utekelezwaji wa mkataba wa amani, kati ya serikali na waasi wa Tigray, uliotiwa saini mwezi Novemba, mwaka uliopita jijini Pretoria nchini Afrika Kusini.

Mbali na kuunga mkono mkataba huo wa amani, Mawaziri hao wamesema wamekuja pia kupigwa debe kutochukuliwa hatua kwa wale waliohusika na vita nchini humo lakini pia kuunga mkono juhudi za ujenzi wa jimbo la Tigray lililoharibiwa na vita.

Ziara hii imekuja, siku moja baada ya waasi wa Tigray kutangaza kuwa wameanza kurejesha silaha nzito walizokuwa wanazitumia wakati wa vita vya miaka miwili na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine kusalia wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.