Pata taarifa kuu
KENYA- AFYA

Kisonono cha kutisha chagunduliwa Nairobi

Watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya KEMRI wanasema kuna aina mpya ya ugonjwa wa kisonono, unaosambaa kwa kasi katika  jiji la Nairobi, hasa miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono wa kike.

Dawa ya kisonono
Dawa ya kisonono today.mims
Matangazo ya kibiashara

Watalaam hao katika utafiti wao, wanalaumu ongezeko hilo kutokana na  taarifa potofu kuwa baadhi ya makahaba ambao wanatumia dawa za kukinga maambukizi ya Ukwimwi, wanaamini kuwa dawa hizo zitawaepusha na magonjwa ya zinaa na hivyo wanashiriki ngomo bila kutumia mpira wa kondomu.

Zaidi ya makahaba 350 kutoka zahanati moja jijini Nairobi, ambayo iliripoti visa vingi vya ugonjwa wa kisonono, walishiriki katika utafiti huo.

Robo tatu ya waliohojiwa, walikiri kufanya mapenzi bila kinga na wapenzi wao na wateja kwani hatua hiyo inalipa zaidi.

Baadhi yao walisema walilala na angalau wateja 29 kwa kipindi cha wiki mbili.

Taasisi hiyo sasa inataka serikali ya Kenya kubadilisha  sera ya sasa ya matibabu pamoja na kuhimiza raia kupimwa zaidi ili kubaini ukubwa wa ugonjwa huo kote nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.