Pata taarifa kuu
UGANDA-AFYA

WHO yatangaza kumalizika kwa Ebola Uganda

Uganda, imetangaza kumaliza kwa maambukizi ya Ebola yaliozuka karibia miezi mitatu iliyopita na kusababisha vifo vya 55.

Wahudumu wa afya wilyani  Mubende, Uganda,
Wahudumu wa afya wilyani Mubende, Uganda, AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa afya katika taifa hilo la Afrika Mashariki Jane Ruth Aceng, akiwa katika wilaya ya Mubende amesema "Tumefaulu kumaliza mlipuko wa Ebola nchini Uganda.”

Kisa cha kwanza cha mgongwa wa Ebola kilithibitishwa katika wilaya hiyo ya Mubende mwezi Septemba mwaka jana.

Hatua hiyo ya kumalizika kwa Ebola nchini Uganda, imethibitishwa na shirika la afya duniani WHO.

Waziri huyo ameeleza kuwa Januari 11 ilihitimisha siku 113 tangu kugunduliwa kwa kisa cha kwanza cha Ebola katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa WHO, taifa hutangazwa kumaliza Ebola iwapo hakujatokea kisa chochote katika kipindi cha siku 42 mtawalia.

Aidha WHO imesema Uganda ilisajili visa 142 vya Ebola, vifo 55, wagonjwa 87 wakiripotiwa kupona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.