Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

Waasi wa CODECO watuhumiwa kutekeleza mauaji ya raia 24 DR Congo

Waasi wanaodhaniwa kuwa ni kutoka kundi la CODECO, wameua watu zaidi ya 24 mwishoni mwa juma lililopita katika vijiji kadhaa kwenye jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi ya DRC.

Ramani ya DRC
Ramani ya DRC RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashirika ya kiraia kwenye eneo hilo, waasi hao walishambulia eneo la Djugu, ambapo walichoma moto nyumba na kuharibu mali nyingine ikiwemo kutekeleza mauji.

Mashirika hayo yamesema, miili mingi ilipatikana katika vijiji vya Jisa, Largu na Blukwa kaskazini mwa jimbo hilo, ambapo baadhi ya maeneo hayajafikiwa huku idadi ya vifo ikitajwa huenda ikaongezeka.

Hata hivyo madai haya ya mashirika ya kiraia yamekanusha na msemaji wa jeshi kwenye eneo la Ituri, Luteni Jules Ngongo, ambaye mbali na kuthibitisha tukio hilo amesema ni watu wanne ndio walikufa akiwemo mwanajeshi mmoja siku ya Jumapili.

Mwanaharakati mmoja wa kutetea haki za binadamu kwenye eneo hilo, Desire Mbutchu, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, waasi wa CODECO walitekeleza mashambulio hayo kama ulipizaji kisasi kwa madai ya kuuawa kwa mwalimu kutoka jamii ya Lendu, ambayo kwa muda sasa wamekuwa katika mzozo na jamii za watu wa Hema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.