Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: M23 waripotiwa kuanza kuondoka Kimbumba

Baadhi ya viongozi kwenye mji wa Kibumba, wameripoti waasi hao kuanza kuondoka ambapo shughuli zimeripotiwa kuanza kurejea katika hali ya kawaida.

Wanajeshi wa Kongo na Kenya nchini DRC
Wanajeshi wa Kongo na Kenya nchini DRC AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Tume ya umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, imetangza kuzinduliwa kwa operesheni maalumu ya kijeshi itakayofahamika kama “LINDA NJIA” (« protège ta route »), lengo likiwa ni kukabiliana na uvamizi wa waasi wa ADF.

Kwa mujibu wa msemaji wake, Ndeye Khady Lo, wanajeshi wao watalinda njia zinazoingia na kutoka mjini Beni hadi Semliki, Kamango na Nobil, maeneo ambayo yanapakana nan chi ya Uganda.

“Ni oparesheni ya muda mfupi inayohusisha MONUSCO na vikosi vya jeshi la Kongo kwa lengo la kuboresha safari za hapa na pale za wanachi.” amesema Ndeye Khady Lo.

Waasi wa ADF wamekuwa wakiripotiwa kutekeleza mashambulio ya raia Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.