Pata taarifa kuu
MALAWI- AFYA

Malawi:Watu 620 wamefariki tangu mwaka jana kutokana na mlipuko wa kipindupindu

Waziri wa afya nchini Malawi Khumbize Chiponda amesema watu 620 wamefariki tangu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kutokea mwaka jana nchini humo.


Mlipuko wa Kipindupindu ulianza nchini Malawi mwezi Novemba karibu na mpaka na nchi ya Tanzania
Mlipuko wa Kipindupindu ulianza nchini Malawi mwezi Novemba karibu na mpaka na nchi ya Tanzania AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kufikia siku ya Jumatatu ya wiki hii , visa 18,222 vya kipindupindu vilikuwa vimeripotiwa, watu 16,780 wakiwa wamepona wakati wengine 822 wakiwa wanapokea matibabu.

Katika taarifa waziri huyo wa afya ameongeza kuwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita, visa  vipya 409 viliripotiwa watu 25 wakidhibitishwa kufariki.

Vituo vyote 29 vya afya  katika wilaya za  nchini humo vimedhibtisha kisa cha maambukizi ya kipindupindu tangu kudhibitishwa kwa kisa cha kwanza cha mgonjwa katika wilaya ya Machinga mwezi Machi mwaka jana.

Siku ya Jumatatu ya wiki hii, serikali nchini humo ilitangaza kuhairisha siku ya kufunguluwa kwa shule za msingi na za upili kwa karibia majuma mawili katika wilaya za Blantyre na Lilongwe.

Muhula mpya ulikuwa umeratibiwa kuuanza Januari 3 ila kutokana na kasi ya maambukizi na vifo serikali ililazimika kuchukua hatua ya kusongeza mbele tarehe ya kufunguliwa kwa shule kama njia moja ya kudhibiti msambao wa maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.