Pata taarifa kuu
UGANDA-AJALI

Uganda: Watoto ni miongoni mwa watu tisa waliofariki kwa mkaganyano

Watu tisa, wenye umri kati ya miaka 10 na 20, wamepoteza maisha jijini Kampala nchini Uganda, baada ya kutokea kwa mkaganyano wa watu, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya, usiku wa kuamkia jana katika jumba la biashara la Freedom City mall. 

Sherehe za kuadhimisha mwaka mpya nchini Uganda
Sherehe za kuadhimisha mwaka mpya nchini Uganda AFP - BADRU KATUMBA
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamesema, watu watano walipoteza maisha papo hapo, huku wanne wakifarifki wakikimbizwa hospitalini kwa kukosa pumzi, katika mkasa ambao pia, ulisababisha majeruhi ya watu kadhaa. 

Polisi wameanzisha uchunguzi katika tukio hilo la usiku wa kuamkia mwaka mpya.

‘‘Polisi wanachunguza kuwepo kwa uzembe na uwamuzi wa haraka kwenye kisa kilichotokea kwenye jumba la freedom mall na kusababisha vifo vya watu tisa wakiwemo watoto saba’’. Amesema Luke Owoyesigyire.

Idadi kubwa ya raia duniani hukusanyika katika maeneo ya umma kusherekea mwaka mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.