Pata taarifa kuu
EAC- AJALI

Watu sita wamefariki katika ajali ya mabasi mawili nchini Uganda

Watu sita wamepoteza maisha nchini Uganda, kufuatia ajali ya barabarani jana jioni iliyohusisha mabasi mawili, moja kutoka Kenya na lingine kutoka Rwanda, katka barabara kuu ya kutoka Ntungamo kwenda Kabale, huku sababu ya ajali hiyo ikielezwa kuwa hali mbaya ya hewa.

Ramani ya Uganda
Ramani ya Uganda Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini Uganda wanasema, katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi na kuelekea kuukaribisha mwaka mpya,zaidi ya ajali 200 zimetokea nchini humo na zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha.

Farida Nampiima, ni msemaji wa idara ya trafiki nchini humo, anaeleza ni kwa nini kumekuwa na ongezeko la ajali kipindi hiki.

“Madereva wengi wanadharau kanuni za usalama barabarani lakini pia wanaendesha magari kwa mwendo wa kasi.”ameeleza Farida Nampiima.

Visa vya ajali za barabarani vimeonekana kuongoza katika baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki katika msimu huu wa sherehe za sikukuu na mwaka mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.