Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI- USALAMA

Sudan Kusini: Watu 30,000 wametoroka makazi yao kutokana na mapigano ya kikabila

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya kibinadamu OCHA, inasema watu zaidi ya Elfu 30 wamekimbia makwao kutokana na ongezeko la mapigano ya kikabila katika jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini.

 Salva Kiir, Rais wa Sudan Kusini
Salva Kiir, Rais wa Sudan Kusini REUTERS - JOK SOLOMUN
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii imetolewa baada ya wiki iliyopita, watu waliojihami kwa silaha, kushambulia eneo la Pibor, huku mapigano mengine yakiripotiwa mwezi uliopita katika jimbo la Upper Nile.

Mwakilishi wa OCHA nchini Sudan Kusini Sara Beysolow Nyanti, amesema mapigano yanayoendelea yanasababisha mateso kwa watoto, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Baadhi ya wanakijiji wamelazimika kutafuta hifadhi misituni na maeneo yenye madibwi ya maji ili kuepuka mauaji yanayoendelea, wakati huu wakihitaji misaada ya kibinadamu kama chakula na dawa.

Umoja wa Mataifa na Shirika la IGAD, limelaani mauaji yanayoendelea na kutaka hatua kuchukuliwa kwa wahusika, wanaochechea mauaji yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.