Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: Zaidi ya raia 20 wameokolewa baada ya kutekwa na waasi wa ADF

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jeshi la nchi hiyo likishirkiana na lile la Uganda, limefanikiwa kuwakomboa watu 22 wakiwemo wanawake 13, huko Beu, Kusini mwa Wilaya ya Irumu, mkoani Ituri, baada ya kutekwa na waasi wa ADF hivi karibuni.

Boga DRC
Boga DRC © baromètre sécuritaire du Kivu
Matangazo ya kibiashara

MAK HAZUKAY, msemaji wa operesheni Shujaa, dhidi ya kundi hilo la waasi, amethibitisha kuokolewa kwa waasi hao hapo jana.

"Kwa Sababu ya presha adui ameacha raia wetu, ukombozi huo unatokana na operesheni zinazo endelea.”ameeleza Mak Hazukay.

Wanajeshi wa FARDC na wale wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wamekuwa wakiendeleza oparesheni kali dhidi ya makundi ya waasi Mashariki wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.