Pata taarifa kuu
BURKINA FASO - USALAMA

U.N: Burkina Faso haina sababu za kumfukuza afisa wetu Barbara Manzi

Umoja wa Mataifa unasema, Burkina Faso haina sababu za kumfukuza afisa wake Barbara Manzi, ambaye ametakiwa kuondoka nchini humo mara moja,akitajwa kuwa mtu asiyetakiwa katika taifa hilo.

 Antonio Guterres katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa AFP - ED JONES
Matangazo ya kibiashara

Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amesema, hatua iliyochukuliwa inasikitisha na kuongeza kuwa maafisa wa Umoja huo wanaweza tu kuondolewa katika nchi husika na wale walioteua.

Kauli hii ya Umoja wa Mataifa inakuja baada ya uongozi wa jeshi hapo jana kutoa taarifa ya kumtaka Manzi, aliyeteuliwa kuwa mwakilishi wa Umoja huo mwaka uliopita, kuondoka kwa shutuma za kulipaka  tope taifa hilo la Afrika Magharibi.

Burkina Faso inasema mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa, amekuwa akitoa ripoti  mbaya kuhusu hali ya usalama, katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikipambana na wanajihadi tangu mwaka 2015.

Waziri wa Mambo ya nje Olivia Rouamba amemstumu pia mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa kwa kutabiri machafuko nchini Burkina Faso katika miezi kadhaa ijayo, matamshi ambayo amesema yanatishia wawekezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.