Pata taarifa kuu
DRC- RWANDA- USALAMA

Rwanda imekana tuhuma kwamba inawaunga M23 mkono baada ya ripoti ya UN

Serikali ya Rwanda, imekanusha kuwasaidia waasi wa M23 mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiitaja ripoti ya wataalamu wa umoja wa Mataifa kama ya uongo na uchochezi.

Rais wa Paul Kagame wa Rwanda na Félix Tshisekedi  wa DRC 25 juin 2021.
Rais wa Paul Kagame wa Rwanda na Félix Tshisekedi wa DRC 25 juin 2021. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano ya kipekee na idhaa ya RFI, msemaji wa Serikali ya Rwanda, Alain Mukuralinda, amekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwa nchi yake.

“Tunasubiri kuangalia ushahidi wanaosema tuufanyie uchunguzi na ndipo tutakapozungumza.” amesema Alain Mukuralinda.

Watetezi wa haki za binadamu wao wanamtazamo gani?

Karl Mweze ni mratibu wa shirika moja la kutetea haki za binadamu jijini Kinshasa.

“Tumesikia mara kwa mara uongozi wa Kigali ukikanusha mara kwa mara kuwa hawako nchini DRC wala hawahusiki na mauaji nchini humo.”amesema Karl Mweze.

Haya yanajiri baada ya hapo jana wataalamu wa umoja wa Mataifa, kudai kwenye ripoti yao kuwa Rwanda imekuwa ikishirikiana na waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.