Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Rais wa Ghana atiwa wasiwasi kuhusu uwepo wa mamluki wa Wagner nchini Burkina Faso

Mamluki wa kampuni ya Wagner kutoka Urusi wako kwa sasa nchini Burkina Faso, kwa mujibu wa rais wa Ghana alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Washington siku ya Jumatano, kando ya mkutano wa rais wa Marekani Marekani na viongozi wa Afrika.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo (wa pili kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika kwenye Ukumbi wa Walter E. Washington Convention Center mjini Washington, Desemba 14, 2022.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo (wa pili kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika kwenye Ukumbi wa Walter E. Washington Convention Center mjini Washington, Desemba 14, 2022. AFP - MANDEL NGAN
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mazungumzo haya, yaliyotangazwa na diplomasia ya Marekani, Nana Akufo-Addo alihakikisha kwamba Burkina Faso, jirani yake wa kaskazini, imehitimisha mpango wa kuitisha kampuni ya mamluki wa Urusi.

Nana Akufo-Addo, mbele ya mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken, amehakikisha kwamba mamluki wa Kirusi tayari wametumwa kwa jirani yake, bila kutoa maelezo ziada.

"Zaidi ya yote, kuna suala ambalo nataka kuliweka mezani haraka. Leo, mamluki wa Urusi wako kwenye mpaka wetu wa kaskazini.

Burkina Faso imekamilisha mpango wake baada ya Mali, wa kuajiri vikosi vya Wagner kwenye ardhi yake. Ninaamini walitengewa mgodi kusini mwa Burkina kama njia ya malipo ya huduma yao. Waziri Mkuu wa Burkina Faso amekuwa Moscow kwa siku kumi zilizopita.

Rais wa Ghana anasikitika kuwa Afrika inageuka tena kuwa ukumbi wa makabiliano kati ya mataifa makubwa, lakini pamoja na kwamba kuzuiliwa kwa Urusi katika bara hilo ilikuwa moja ya malengo ya mkutano huu wa Umoja wa Marekani na Afrika, hakusita kuwaomba Marekani kuonyesha uungaji mkono wake.

"Mbali na kutokubali kuona mataifa makubwa makubwa yakiifanya Afrika kuwa ukumbi wao wa shughuli tena, pia tumekuwa na msimamo wazi kuhusu vita vya Ukraine: mara kwa mara tumekuwa tukilaani hadharani uvamizi wa Urusi. Hivyo kuwa na kundi hili kwenye mpaka wetu ni jambo linatia wasiwasi.

Na ningependa mjadala huu uendelee: ni kwa kiasi gani tunaweza kuwa na nchi hii kama mshirika katika kukabiliana na hatari hii? Ni muhimu sana,” alisema Nana Akufo-Addo katika mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Msemaji wa serikali ya Burkina Faso hakutaka kujibu madai haya. "Ninamwachia jukumu la kile alichosema," alijibu Jean-Emmanuel Ouedraogo kwa shirika la habari la AFP.

Katika mahojiano na Jeune Afrique, mnamo Desemba 14, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, kwa upande wake alizungumzia "uvumi" uiliozagaa wa kutumwa kwa mamluki wa Wagner nchini Burkina Faso, uvumi ambao ambao alisema unatia 'wasiwasi mkubwa.'

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.