Pata taarifa kuu
RWANDA- SIASA.

Kagame: Hakuna yeyote duniani, anayeweza kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu

Rais wa Rwanda, Paul Kagame akizungumza pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani, amesema hakuna yeyote duniani, anayeweza kuingilia mambo ya ndani ya nchi yake, wakati huu akipata shinikizo kutoka kwa Marekani, kumwachilia huru, Paul Rusesabagina mkosoaji wa serikali yake, ambaye amefungwa jela miaka 25 kwa makosa ya ugaidi. 

Paul Kagame,rais wa Rwanda
Paul Kagame,rais wa Rwanda REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Rais Kagame amesisitiza kuwa mambo ya ndani ya taifa lake yatatatuliwa na suluhisho kutoka ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki

“Tumeweka wazi kabisa hakuna mtu yeyote, pale popote atakayekuja kutushurutisha kuhusu nini cha kufanya na maisha yetu.” amesema rais Kagame.

Kauli hii ya Kagame, imekuja wakati huu, Marekani ikiitaka Rwanda kumwachia Rusesabagina aliyejipatia umaarufu baada ya kuwaisadia mamia ya watu ndani ya hoteli aliyokuwa anaifanyia kazi, wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994. 

Wanaharakati na familia ya Rusesabagina, wanasema kesi dhidi yake imechochewa kisiasa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.