Pata taarifa kuu

Tshala Muana, nguli wa Rumba ya Kongo afariki dunia

Elizabeth Tshala Muana, nguli wa Rumba ya DRC, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 64, kulingana na VOA ikinukuu chanzo rasmi.

@ Anabelle Jogama-Andy
Matangazo ya kibiashara

“Tshala Mwana amefariki dunia Jumamosi hii ya tarehe 10/12. Tutakumbuka dhamira yake ya kutetea maslahi ya kitaifa na Afrika, Rumba yake iliyochanganyika na mila ya Waluba na aliimba nyimbo nyingi ambazo zilipendwa na kupata sifa kama vile Lwatuye, Karibu yangu, Nasi nabali na nyingine) yenye mafunzo ya maadili, ' Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya DRC imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Habari hizo zimethibitishwa kwanza na mshirika wake wa maisha, mwanasiasa Claude Mashala.

"Asubuhi na mapema Mola Mwema Alichukua uamuzi wa kumchukua Mamu Tshala Muana. Mungu Mwema Atukuzwe kwa nyakati zote njema Alizotujalia hapa duniani. Kwaheri Mamu kutoka kwangu" , amesema Claude Mashala kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Ndugu wengine wamethibitisha kuwa mwanamuziki huyo alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya mtaani usiku baada ya kuugua.

Tshala Muana anayejulikana kwa Rumba iliyochanganyikana na maneeo ya Kiluba, alikuwa aanajishughulisha na siasa kwa miaka kadhaa.

Mara nyingi aliwaimbia wanasiasa wakati wa kampeni za uchaguzi. Alimtengenezea nyimbo Rais wa zamani Laurent-Désiré Kabila lakini pia mtoto wake Joseph Kabila ambaye alimrithi baba yake.

Miaka mitatu iliyopita, moja ya nyimbo zake, "Kutokuwa na shukrani", ilimfanya akamatwe na vyombo vya usalama. Aliachiliwa baada ya kueleza kuwa haikuwa ikimkosoa Rais wa sasa Felix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.