Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

Mateka waliokuwa wanashikiliwa na waasi wameachiwa huru nchini DRC

 Zaidi ya raia 57 waliokuwa wametekwa nyara na makundi ya waasi mashariki mwa nchi ya DRC, wengi wakiwa vijana wakike waliotumikishwa kama watumwa, wameungana na familia zao.

Wanajeshi wa  FARDC wakitoa ulinzi kwa magari ya raia yaliobeba bidhaa kutoka Beni kuelekea Komanda.
Wanajeshi wa FARDC wakitoa ulinzi kwa magari ya raia yaliobeba bidhaa kutoka Beni kuelekea Komanda. © Sebastien Kitsa Musay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vijana hawa waliachiwa wiki iliyopita baada ya operseheni zilizofanywa kwa pamoja na wanajeshi wa Serikali FARDC na wale wa Uganda, UPDF kulenga ngome za waasi wa ADF.

Operesheni za pamoja kati ya Uganda na DRC dhidi ya waasi wa ADF zimekuwa zikutekelezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa mashariki mwa nchi hiyo.

Mateka hao ambao wengi ni wanawake, waliunganishwa na familia zao katika sherehe zilizofanyika mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini.

Kundi la waasi wa ADF ambalo linauhusiano na Islamic State, linatuhumiwa kutekeleza vitendo vya mauaji na utakaji mashariki mwa nchi hiyo na katika ardhi ya Uganda.

Haya yanajiri wakati huu ripoti zikionesha kuwa maelfu ya raia mashariki mwa DRC wameendelea kushikiliwa mateka, huku watoto waliokamatwa wakitumikishwa kama wapiganaji, ambapo eneo hilo lina zaidi ya makundi ya waasi 100.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.