Pata taarifa kuu

Mapigano DRC: Mkutano kati ya wakuu wa diplomasia ya Marekani na Rwanda wafanyika

Mashariki mwa DRC, hali ya utulivu inatawala Jumatano hii, Novemba 16 baada ya siku kadhaa za mapigano makali kati ya jeshi la DRC, FARDC, na waasi wa M23. Waasi hawa kwa sasa wako kama kilomita ishirini kaskazini mwa mji wa Goma, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini. 

Hofu ikitanda katika kambi ya wakimbizi ya Kanyaruchinia, kwenye lango la Goma, Jumanne, Novemba 15, 2022. Sehemu kubwa ya familia zilizopata hifadhi huko zilikimbia, wakihofia kushambuliwa na M23.
Hofu ikitanda katika kambi ya wakimbizi ya Kanyaruchinia, kwenye lango la Goma, Jumanne, Novemba 15, 2022. Sehemu kubwa ya familia zilizopata hifadhi huko zilikimbia, wakihofia kushambuliwa na M23. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka za Kongo zinadai kushikilia ngome zao, wakati jitihada kadhaa za kidiplomasia zimeshuhuduwa. Kando ya mkutano wa nchi tajiri, G20, mjini Bali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alikutana na mwenzake wa Rwanda na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akazungumza kuhusu mzozo huo.

"Nilikuwa na mkutano muhimu na Vincent Biruta. Nilisisitiza wasiwasi mkubwa wa Marekani kuhusu kuendelea kwa ghasia mashariki mwa DRC, na kuitaka Rwanda kuchukua hatua ili kuwezesha kukoma kwa uhasama huu,” Antony Blinken ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, akiambatanidha na picha zinazomonyesha akizungumza na waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda katika Hoteli moja.

"Nilisisitiza ushiriki wa Rwanda katika mifumo ya kikanda kuleta amani na utulivu katika kanda, na kusisitiza haja ya washikadau wote kufanyia kazi suluhu ya kisiasa katika zzozo huo."

Emmanuel Macron: kipaumbele "kujihusisha tena katika mchakato wa kisiasa"

Ufaransa, kwa upande wake, imesisitiza kuunga mkono mchakato wa Nairobi. Hivi ndivyo Emmanuel Macron amekumbusha, akihojiwa juu ya mada hiyo na mwandishi wetu maalum katika mkutano wa G20 Mounia Daoudi. "Ninaamini, kuna njia inayowezekana, inayohusisha kanda kwa misingi ya mchakato wa Nairobi, ambao tunaunga mkono, kutumwa kwa vikosi vya kikanda ili kuweza kuleta utulivu katika miji kadhaa, hasa Bunagana, na hivyo kuruhusu kuondoka kwa waasi wa M23, na zaidi ya yote kuweza kujihusisha tena katika mchakato wa kisiasa, ambao lazima uwe kipaumbele katika kushughulikia mivutano hii. "

Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza kuwa mazungumzo mapya yatafanyika Novemba 21 jijini Nairobi. Mpatanishi, Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, alikuwa Goma siku ya Jumanne, ambapo gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, Jenerali Constant Ndima, aliwatolea wito wakazi kuwa "watulivu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.