Pata taarifa kuu

Rais wa Angola mjini Kigali kwa upatanishi kati ya Rwanda na DRC

Rais wa Angola Joao Lourenco amewasili nchini Rwanda siku ya Ijumaa kujaribu kutafuta suluhu ya kidiplomasia kati ya Kigali na Kinshasa kuhusu kuzuka upya kwa mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yanayosisha makundi mengi yenye silaha.

Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa kilele wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC.
Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa kilele wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC. AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya hivi majuzi ya M23, waasi wa zamani wa Kitutsi ambao walichukua silaha tena mwishoni mwa mwaka 2021, yalifanya kundi hilo likisonga mbele kuelekea Goma, jiji kuu katika eneo hilo, na kuchochea mvutano kati ya DRC na Rwanda. Kinshasa inaishutumu Kigali kwa kuunga mkono M23, jambo ambalo mamlaka ya Rwanda inakanusha.

Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, mamlaka ya Kongo ilimfukuza balozi wa Rwanda.

Baada ya wiki kadhaa za utulivu, waasi wa M23 walianza tena mashambulizi Oktoba 20, wakateka maeneo kadhaa katika eneo la Rutshuru (Kivu Kaskazini), ikiwa ni pamoja na Bunagana, mji wa kimkakati kwenye mpaka na Uganda, na kuteka maeneo kwenye barabara inayohudumia mji mkuu wa mkoa, Goma.

Rais wa Angola, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), atakutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame "kama sehemu ya juhudi za kikanda za kurejesha uhusiano kati ya Rwanda na DRC," gazeti la chama tawala cha Rwanda, The New Times, ilimeripoti siku ya Ijumaa.

Mwambata wa Rais wa Rwanda, Stéphanie Nyombayire, amethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba Paul Kagame atakutana na Bw. Lourenço ambaye amewasili Ijumaa. Makubaliano ya kumaliza uhasama uliandaliwa katika mkutano wa kilele uliosimamiwa na Angola kati ya Paul Kagame na mwenzake wa Kongo Felix Tshisekedi mwezi Julai.

Bunge la Kenya Jumatano liliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi 903 kama sehemu ya kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki ili kuleta utulivu mashariki mwa DRC.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 188,000 wamekimbia vijiji vyao tangu Oktoba 20 na "kuhamia maeneo tulivu" katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Takriban wengine 16,500 wamekimbilia nchini Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.