Pata taarifa kuu
UCHUMI-HAKI

Mshahara wa wabunge DRC: Wabunge wawili wa upinzani wasikilizwa na tume ya bunge

Wabunge wawili wa upinzani Jean-Baptiste Kasekwa na  Delly Sesanga, wamesikilizwa na Tume ya bunge kuhusu madai waliyotolewa kuwa wabunge wanalipwa kila mwezi Dola Elfu 21, kiwango cha fedha ambacho hakijawahi kuwekwa wazi na uongozi wa bunge.

Moja ya vikao vya Bunge la Kitaifa la DRC.
Moja ya vikao vya Bunge la Kitaifa la DRC. JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Madai hayo yalizua mjadala nchini humo kuhusu kiwango cha mishahara cha wabunge, kinachoelezwa kuwa kikubwa. 

Baada ya kuhojiwa, mmoja wabunge hao Delly Sesanga, alisistiza kuwa ana ushahidi wa madai aliyotoa. 

Nilirejelea upya mapato yote niliyopokea kwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na sehemu iliyohusishwa na malipo ya kodi ya viongozi waliochaguliwa. Na ninaweza kuwahakikishia kuwa nina ushahidi wa kutosa kuhusu viwango vilivyofikiwa.

Mbunge huyo amekumbusha kwamba "malipo ya mbunge ni pamoja na sio tu sehemu ya mishahara, lakini pia marupurupu mengine zote".

Pingamizi

Tume italazimika kuwasilisha ripoti yake na hati ya mashtaka ambayo itajadiliwa na kupigiwa kura katika kikao. Lakini wabunge hao wawili ambao wanashutumu hali ya kutotulia kisiasa tangu mwanzo wa suala hili, wanapinga uhalali wa tume iliyoundwa.

Kwa mujibu wa Delly Sesanga, ni Kamati ya Wazee wa Bunge pekee ndiyo yenye uwezo wa kushughulikia suala la kinidhamu. Wabunge hao wawili wana hatari ya kusimamishwa kazi kwa miezi kadhaa kwa kunyimwa mishahara au kulazimishwa kuwasilisha ombi la msamaha kwa umma, kulingana na mjumbe wa kamati maalum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.