Pata taarifa kuu

DRC: 10 wafariki katika tamasha la Fally Ipupa, Kinshasa

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaomboleza vifo vya raia wake kumi na mmoja waliofariki jana Jumamosi katika mkanyagano wakati wa tamasha la muziki la Fally Ipupa. Mamlaka zimesema watu wengi walikufa kwa kukosa pumzi wakati wa mkasa huo.

Picha ya tamasha la Fally Ipupa, ambapo watu walikufa katika mkanyagano, katika uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa, Oktoba 29, 2022.
Picha ya tamasha la Fally Ipupa, ambapo watu walikufa katika mkanyagano, katika uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa, Oktoba 29, 2022. REUTERS - PAUL LORGERIE
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu kumi na mmoja walifariki Jumamosi, Oktoba 29, katika mkanyagano wakati wa tamasha la mwanamuziki nguli wa DRC, Fally Ipupa, katika uwanja mkubwa zaidi wa michezo wa Martyrs katika mji mkuu, Kinshasa. Watazamaji tisa na maafisa wawili wa polisi walikufa, polisi imetangaza Jumapili asubuhi, baada ya usiku msukosuko.

Ilikuwa ni moja ya matukio yaliyotarajiwa sana na wapenzi wa muziki wa Kongo kwa wiki nyingi huko Kinshasa, lakini tukio hilo liligeuka kuwa la kusikitisha. Mamlaka zinaonyesha dosari katika maandalizi ya tamasha hilo.

Uwanja ulikuwa umejaa. Watazamaji waliwekwa hata chini na wengine walirundamana kwenye barabara za ukumbi wa uwanja.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na maandamalizi ya tamasha hilo, zaidi ya watu 120,000 ndio walikuwa kwenye uwanja huo wakitazama tamasha hilo . Bado haijajulikana ni nini kilisababisha mkanyagano huo, lakini watazamaji kadhaa walizimia kabla na wakati wa tamasha hilo.

Asubuhi ya Jumapili hii, Daniel Aselo, Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia Mambo ya Ndani, aliwahoji waandaaji ambao kwa mujibu wake, hawakuheshimu ahadi zao, hasa katika suala la uwezo wa mapokezi.

"Watu walikosa hewa. Hakuna aliyepigwa. Katika tukio hili, mratibu wa tamasha hilo lazima ashtakiwe na kuadhibiwa. Anatakiwa kujitokeza na kuieleza Jamhuri kwa nini alipanga vibaya tamasha hili lililosababisha watu kupoteza maisha,” amesema.

Kulingana na Daniel Aselo, mjumbe wa kamati ya maandalizi alikamatwa asubuhi ya Jumapili na wengine wanaendelea kusakwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.