Pata taarifa kuu

Niger: takriban raia 11 wameuawa katika mashambulizi karibu na mpaka wa Mali

Takriban raia 11 waliuawa Jumamosi magharibi mwa Niger wakati lori tatu na pikipiki zilishambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu", karibu na mpaka na Mali, afisa wa manispaa kutoka Banibangou, mji ambapo mashambulizi yalifanyika, ameliambia shirika la habari la AFP.

Wasu sojojin jamhuriyar Nijar da ke taimakawa Najeriya wajen yaki da kungiyar Boko Haram.
Wasu sojojin jamhuriyar Nijar da ke taimakawa Najeriya wajen yaki da kungiyar Boko Haram. AFP - PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

"Malori matatu yalizuiliwa siku ya Jumamosi mwendo wa saa tano mchana na watu wenye silaha na maafisa tisa waliokuwemo (...) wote waliuawa. Watu wengine wawili waliokuwa kwenye pikipiki pia waliuawa,” afisa wa manispaa ameliambia shirika la habari la AFP. Mbunge wa eneo hilo amethibitisha idadi ya waliofariki kuwa kumi na moja.

Malori hayo matatu yalishambuliwa kwenye barabara ya mchanga na isiyo na watu kati ya mji wa Banibangou na eneo la Tizigorou, karibu na mpaka wa Mali. Lori moja lilikuwa limetoka tu Banibangou ambako lilikuwa lilipeleka saruji kwa wanakandarasi siku ay Ijumaa. "Kulingana na taarifa tulizo nazo, watu kumi na mmoja ndio waliuawa, malori mawili yalichomwa moto na jingine kubebwa," mbunge kutoka eneo hilo amelithibitishia shirika la habari la AFP.

Mashambulizi haya yanakuja baada ya miezi kadhaa ya utulivu katika eneo la Banibangou, karibu na mpaka wa Mali ambapo watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi walizidisha mashambulizi ya umwagaji damu dhidi ya raia katika vijiji vyao na katika mashamba yao tangu 2021.

Mwezi Februari mwaka jana, watu 18 waliuawa katika shambulizi dhidi ya lori la uchukuzi lililotekelezwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika eneo la Banibangou. Mnamo Novemba 2, 2021, angalau maafisa 69 wa Kamati ya kujihami (wanamgambo), wakiongozwa na meya wa Banibangou, waliuawa na watu wenye silaha, kulingana na mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.