Pata taarifa kuu

Tigray: HRW lataka kuchukuliwa vikwazo kwa komesha mapigano

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) Jumatano limetoa wito wa kuwekewa vikwazo kwa baadhi ya watu na vikwazo vya silaha katika kukabiliana na hatari kubwa kwa raia katika eneo la waasi la Tigray nchini Ethiopia kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na vikosi vya serikali na vile kutoka Eritrea.

"Hali nchini Ethiopia inazidi kudorora," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema.
"Hali nchini Ethiopia inazidi kudorora," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku kadhaa za mashambulizi ya angani yaliyoua raia kadhaa, akiwemo afisa wa shirika hilo lisilo la kiserikali la kibinadamu, vikosi vya Ethiopia na Eritrea viliuteka mji muhimu wa Shire siku ya Jumatatu, uliokuwa na wakazi wapatao 100,000 kabla ya kuanza kwa vita mnamo mwezi Novemba 2020 na kuwapa hifadhi watu wengi kutoka jimbo la Tigray waliohamishwa na vita. Mamlaka pia inadai kuchukua udhibiti wa maeneo ya Alamata na Korem kusini mwa Tigray.

"Mateso ya raia nchini Ethiopia lazima yaache kuvumiliwa kwa manufaa ya kisiasa," HRW imesema katika taarifa, ikitoa wito kwa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) kuchukua hatua "zinazofaa", ikiwa ni pamoja na vikwazo dhidi ya baadhi ya watu na vikwazo vya silaha.

Siku ya Jumanne, Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, aliripoti "umati mkubwa wa watu unaelekea katika mji wa Shire", hali ambayo "inazidisha hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari ipo" na "inaleta hatari zaidi ya unyanyasaji dhidi ya raia".

Kulingana na Stéphane Dujarric, takriban watu milioni 2.5 wamekimbia makazi yao huko Tigray na mikoa jirani ya Amhara na Afar, ambapo mzozo umeenea. "Hali mbaya nchini Ethiopia inazidi kutawala," Guterres mwenyewe alisema siku moja kabla.

"Kukiri" huku kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa "kunalazimisha zaidi Baraza la Usalama kushughulikia hali hiyo", imesisitiza HRW.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.