Pata taarifa kuu

Ituri: Watu 120,000 waliokimbia makazi yao wapewa ulinzi na walinda amani wa UN Djugu

Vikosi vya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, wanatoa ulinzi kwa takriban watu laki moja na ishirini elfu waliokimbia makazi yao katika maeneo mbalimbali ya eneo la Djugu.

Askari wa jeshi la Umoja wa mataifa wakipiga kambi katika eneo la Lita huko Djugu, Ituri Machi 27, 2018.
Askari wa jeshi la Umoja wa mataifa wakipiga kambi katika eneo la Lita huko Djugu, Ituri Machi 27, 2018. ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika eneo la Bule, waliokimbia makazi na wenyeji wanasema wanafanya kazi kila siku na kwa amani katika hekta kadhaa za mashamba yanayozunguka kambi ya MONUSCO. Wanakadiriwa kuwa zaidi ya watu elfu themanini waliowekwa katika maeneo matatu.

Katika maeneo ya Jaiba na Jina, Kambi ya  waliolazimika kuyahama makazi yao imejengwa mita 10 kutoka kambi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa, wengi wao wamesema.

Wengi wa waliokimbia makazi yao ni wanawake na watoto.

Kwa watu hawa waliokimbia makazi yao, kuishi kwao kunategemea hasa walinda amani wanaowalinda dhidi ya mashambulizi ya wanamgambo wa CODECO. "Bila MONUSCO, hatungeweza kuishi hapa" , waemesema wegi wa watu hao.

Wameoma vikosi vya Umoja wa Mataifa kuendelea kuwapa ulinzi hadi pale amani itarejea katika vijiji vyao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.