Pata taarifa kuu

Tigray: Mazungumzo ya amani kufanyika Afrika Kusini

Serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray wamesema wako tayari kusafiri kwa mazungumzo nchini Afrika Kusini kwa mwaliko wa Umoja wa Afrika.

Mpiganaji xa kundi la waasi la Tigray Peoples Liberation Front nje ya mji wa Hawzen mnamo Mei 7, 2021.
Mpiganaji xa kundi la waasi la Tigray Peoples Liberation Front nje ya mji wa Hawzen mnamo Mei 7, 2021. © AP Photo/Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Jana Jumatano Serikali ya Ethiopia ilisema, imekubali ombi la Umoja wa Afrika, kushiriki kwenye mazungumzo ya amani na waasi wa Tigray, kujaribu kumaliza mapigano ambayp yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili. 

Redwan Hussein, mshauri wa masuala ya usalama kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed kupitia ukurasa wake wa Twitter, alithibitisha serikali kukubali ombi hilo akisema inaendana na msimamo wa serikali wa kutaka mzozo huo kutatuliwa kwa amani. 

Umoja wa umesema mazungumzo hayo yatafanyika wikendi hii. 

Kiongozi wa waasi wa Tigray amesema yuko tayari kutuma wajumbe kushiriki mazungumzo nchini Afrika Kusini lakini ataomba kujuwa mazungumzo hayo yatafanyika katika mazingira gani.

Ripoti za kidiplomasia zinasema, mazungumzo hayo yataongozwa na mjumbe wa Umoja wa Afrika kwenye ukanda wa pembe ya Afrika, rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanja na aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.