Pata taarifa kuu

Ethiopia: Bei ya mafuta yapanda kwa mara nyingine 20%

Bei ya mafuta nchini Ethiopia imepanda kwa takriban 20% siku ya Alhamisi, chini ya miezi mitatu baada ya kupanda hapo awali kwa 30% hadi 40%, kama sehemu ya kufuta ruzuku ya serikali kwa bidhaa za petroli.

Serikali - ambayo ina ukiritimba wa uagizaji wa mafuta, yanayosafirishwa kwa barabara kutoka Djibouti hadi Ethiopia, ilikuwa tayari imepandisha bei ya rejareja mnamo mwezi Desemba 2021 na tena mwezi Mei 2022.
Serikali - ambayo ina ukiritimba wa uagizaji wa mafuta, yanayosafirishwa kwa barabara kutoka Djibouti hadi Ethiopia, ilikuwa tayari imepandisha bei ya rejareja mnamo mwezi Desemba 2021 na tena mwezi Mei 2022. © Amanuel Sileshi / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ghafi mwaka huu, ambayo yanaongeza nakisi ya serikali, serikali ya Ethiopia imeamua kuondoa hatua kwa hatua ruzuku zote za mafuta tangu mwezi Julai.

"Ingawa bei za mafuta za kimataifa zimeonyesha uthabiti fulani mnamo mwezi Septemba, tofauti bado ni kubwa ikilinganishwa na zile za nchi yetu," kulingana na Wizara ya Biashara katika taarifa iliyotolewa Jumatano jioni.

Ili "kuambatana na soko la kimataifa, bei mpya zimetangazwa" siku ya Alhamisi, kulingana na wizara.

Bei ya petroli imeongezeka kwa 19.83%, kutoka birr (pesa za Ethiopia) 47.83 hadi birr 57.05 (sawa na euro 1.12), na ile ya dizeli na mafuta ya taa imeongezeka kwa 22.19%, kutoka birr 49.02 hadi birr 59.90 (sawa na euro 1.18).

Kwa jumla, mwezi tangu Desemba, bei ya petroli na dizeli nchini Ethiopia imeongezeka zaidi ya mara mbili, ikiongezeka kwa 120% na 157% mtawalia.

Ruzuku ya mafuta hupitiwa upya kila baada ya miezi mitatu.

Hatua ya kwanza ya kuondoa ruzuku mwezi Julai ilisababisha bei ya petroli kupanda kwa karibu 30% na ile ya dizeli kwa karibu 40%.

Serikali - ambayo ina ukiritimba wa uagizaji wa mafuta, yanayosafirishwa kwa barabara kutoka Djibouti hadi Ethiopia, ilikuwa tayari imepandisha bei ya rejareja mnamo mwezi Desemba 2021 na tena mwezi Mei 2022.

Kulingana na wachambuzi, mzozo katika eneo lenye upinzani la Tigray, ambao umedumu kwa miaka miwili, unaelemea uchumi wa Ethiopia, kutokana na gharama yake kwa fedha za umma na kusita kwa wafadhili na wawekezaji wa kimataifa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.