Pata taarifa kuu

UN yatoa wito wa 'kuachiliwa mara moja' kwa wanajeshi wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa Mali

Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa imetoa wito katika taarifa siku ya Jumatatu wa "kuachiliwa mara moja" kwa wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa nchini Mali tangu mwanzoni mwa mwezi wa Julai mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 20, 2022.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 20, 2022. © AP/Mary Altaffer
Matangazo ya kibiashara

Sekretarieti hiyo, inayojumuisha miundo ya siku hadi siku ya uongozi wa Umoja wa Mataifa akiwemo Katibu Mkuu Antonio Guterres, "inataka kuachiliwa mara moja kwa wanajeshi wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa, kwa nia ya uhusiano wa kindugu kati ya watu wa Côte d'Ivoire na Mali. ".

"Inaunga mkono kwa nguvu juhudi zote za kuwezesha kuachiliwa huku pamoja na kurejesha uaminifu na kukuza ujirani mwema kati ya nchi hizo mbili", imeongeza taarifa hiyo, ikisisitiza "kuthamini sana mchango wa Côte d'Ivoire katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa na kwa MINUSMA (ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali) hasa".

Kukamatwa kwa wanajeshi hao wa Côte d'Ivoire mnamo Julai 10 huko Bamako na kufunguliwa mashtaka katikati ya mwezi wa Agosti kwa "jaribio la kuhatarisha usalama wa Mali" kuligeuka kuwa mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili jirani.

Utawala wa kijshi wa Mali wanawona wanajeshi hawa kama "mamluki" huku Abidjan ikihakikisha kwamba walikuwa kwenye misheni ya Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya shughuli za msaada wa vifaa kwa MINUSMA.

Wakati wa mahojiano wiki iliyopita na RFI na France 24, Antonio Guterres alitangaza kwamba wanajeshi wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa hawakuwa "mamluki", na kuibua hasira ya jeshi la Mali.

Wakati wa hotuba yake Jumamosi kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Kanali Abdoulaye Maïga, kaimu Waziri Mkuu wa Mali, alimshambulia Katibu Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.