Pata taarifa kuu

Rais wa DRC aishtumu Rwanda kuunga mkono M23, Kigali yakanusha

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Thisekedi kwenye hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameishtumu tena Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M 23, ambao wameendelea kuudhibiti mji wa Bunagana, Mashariki mwa nchi yake.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Rais wa DRC Félix Tshisekedi (kushoto), mjini Rubavu, Rwanda, Juni 25, 2021.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Rais wa DRC Félix Tshisekedi (kushoto), mjini Rubavu, Rwanda, Juni 25, 2021. © AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Sehemu kubwa ya hotuba yakeilijikita kwenye kuelezea jinsi ukosefu wa usalamaunavyoendelea kuiadhibu nchi yake kwa miongo kadhaa sasa, akifananisha mifumo na makubaliano yote ya kurejesha amani kama jengo lililojengwa juu ya msingi mbovu na hivyo kutokuwa na budi ya kuporomoka.

Thisekedi pia ameshtumu jeshi la Rwanda kwa kushirikiana na waasi hao walioangusha ndege ya Umoja wa Mataifa mwezi Machi, na kusababisha vifo vya watu wanane.

Tshisekedi alisema Wakongo wameshachoka na hali hii inayojirejea miaka nenda miaka rudi na sasa wanataka uthabiti na udhibiti kamili ya nchi yao.

Rais wa DRC amesisitiza jukumu la taifa hilo jirani kwenye msiba unaowakumba Wakongo kwenye maeneo ambayo jeshi la Rwanda na wapiganaji wa M23 wanakutikana mashariki mwa Kongo.

M23 ni washirika wa Kigali na Tshisekedi alitumia ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa kuthibitisha tuhuma zake hizo, akisema kwamba suala la kuhusika kwa Rwanda kwenye uungaji mkono wake kwa M23 si jambo tena la kubishaniwa. 

Rwanda, imeendelea kukanusha madai ya DRC na kiongozi wake Paul Kagame, anatarajiwa kuuhutubia mkutano huo baadaye hivi leo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.