Pata taarifa kuu
UFISADI-HAKI

Mshauri wa rais wa DRC Vidiye Tshimanga aachia ngazi kufuatia kashfa ya rushwa

Mshauri wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amejiuzulu baada ya mkanda wa video kumwonesha, akiahidi kusaidia uwekezaji katika sekta ya madini iwapo, atapata mgawo wa fedha. 

Vidiye Tshimanga, mshauri huyo wa rais Felix Tshisekedi, aliyejiuzulu kufuatia kashfa ya rushwa.
Vidiye Tshimanga, mshauri huyo wa rais Felix Tshisekedi, aliyejiuzulu kufuatia kashfa ya rushwa. © YouTube / Le Temps
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Uswisi la Le Temps limeripoti kuwa, Vidiye Tshimanga, mshauri huyo wa rais Felix Tshisekedi, alimwahidi watu ambao hawakufahamika, wanaominiwa ni wewekezaji kutoka Hong Kong, kuwa atalinda masilahi yao nchini DRC, iwapo watamlipa fedha, kwa mujibu wa mkanda huo ulioonekana. 

Katika mkanda huo, anasikika akisema kuwa, yeye ni mshirika wa karibu sana wa rais Tshisekedi na alifadhili kampeni za kugombea urais, na akimwomba chochote anampa. 

Mkanda huo, umezua hasira miongoni mwa raia wa DRC kwenye mitandao ya kijamii, na kumshinikiza mshauri huyo kujiuzulu, huku Ofisi ya rais ikionya kuwa yeyote atakayepatikana akishiriki kwenye ulaji rushwa, atachukuliwa hatua. 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inayojivunia utajiri wa madini mbalimbali, inaendelea kutajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vibaya kwenye vita dhidi ya ufisadi, na inayoorodheswa katika nafasi ya 169 kati 180 kwenye orodha bora ya nchi zinazopambana na janga hilo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.