Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Uchaguzi Angola: CNE yatangaza ushindi wa MPLA, Rais Lourenço achaguliwa tena

Chama tawala cha kihistoria cha Angola kimeshinda uchaguzi wa wabunge, na kumpa Rais aliye madarakani João Lourenço muhula wa pili, kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa siku ya Jumatatu (tarehe 29 Agosti).

Mgombea anayewania tena kiti cha urais, Rais wa sasa wa Angola João Lourenço wakati wa kampeni za uchaguzi ya chama cha MPLA, Agosti 20, 2022.
Mgombea anayewania tena kiti cha urais, Rais wa sasa wa Angola João Lourenço wakati wa kampeni za uchaguzi ya chama cha MPLA, Agosti 20, 2022. © AFP - JULIO PACHECO NTELA
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa katika historia ya nchi hiyo, chama cha Popular Movement for the Liberation of Angola (MPLA) kimeshinda kwa asilimia 51.17 ya kura zilizopigwa, dhidi ya 43.95% za chama cha kwanza cha upinzani,  National Union for the Total Independence of Angola (Unita), Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Unita, chama cha Adalberto Costa Junior, 60, kimepinga matokeo ya awali, ambayo tayari yamekipa chama tawala cha MPLA ushindi. Maafisa watano wa CNE pia walitishia kutotia saini matokeo ya mwisho.

Chama cha MPLA, ambacho kilishinda mwaka wa 2017 kwa 61% ya kura, kimepata kura ndogo zaidi maka huu. Mnamo 2012, kilipata 71.84% ya kura. Kinashikilia wingi wa viti Bungeni kikiwa na viti 124 kati ya 220. Lakini kinapoteza theluthi mbili ya kura ambayo hadi sasa haitakiwezesha kupitisha sheria bila kuungwa mkono na chama kingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.