Pata taarifa kuu

Mkuu wa diplomasia ya Ujerumani ziarani nchini Morocco kufufua uhusiano

Akiwa ameandamana na manaibu na maafisa kadhaa kutoka wizara yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, atakutana na mwenzake wa Morocco Nasser Bourita, mjini Rabat, Alhamisi hii, Agosti 25. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa mjini Rabat akiambatana na manaibu na maafisa kadhaa kutoka wizara yake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa mjini Rabat akiambatana na manaibu na maafisa kadhaa kutoka wizara yake. © Bernd von Jutrczenka/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili sasa zinataka kuimarisha ushirikiano wao wa pande mbili katika maeneo kadhaa, baada ya kudorora kwa uhusiano, hali iliyoanza mwanzoni mwa mwaka huu. Kulingana na vyanzo vya Morocco, makubaliano ya nchi mbili yatafanyika hasa kwenye nyanja ya nishati ya kijani.

Kufunga ukurasa wa mgogoro kati ya nchi hizo mbili uliotokea Machi 2021 baada ya Kansela Olaf Scholz kuingia madarakani ndilo lengo kuu la ziara hii, ambayo inalenga kuzindua upya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ushirikiano kwenye nyanja za nishati utakuwa katikati ya ziara hii, hasa kuhusu hidrojeni ya kijani. Morocco inaweza kuanza uzalishaji katika eneo hili ndani ya miaka mitatu, na mipango ya kuuza nje bidhaa zake. Berlin iliruhusu safari yake ya kwanza siku ya Jumatano kwa treni 14 zinazotumia hidrojeni na Wajerumani wanatafuta vifaa kwa ajili ya teknolojia hiyo ya kibunifu.

Kama ukumbusho, Rabat ilikuwa imezuia uhusiano wake na Ujerumani, kutokana na "kutoelewana kwa kina" na Berlin kuhusu suala la Sahara Magharibi. Mfalme wa Morocco alitangaza wiki iliyopita kwamba Sahara ni "eneo ambalo Morocco inazingatia mazingira yake ya kimataifa".

Mvutano kati ya Rabat na Berlin ulitulia baada ya barua iliyotumwa na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kwa Mfalme Mohammed VI. Katika barua hii, Bw. Steinmeier alitaja kwamba mradi wa Rabat wa uhuru wa Sahara Magharibi ni "msingi mzuri" ambao unaonyesha "juhudi kubwa" za ufalme huo kwa ajili ya ufumbuzi wa mgogoro huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.