Pata taarifa kuu
KENYA- AJALI.

Kenya: Zaidi ya watu 30 wamefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea Jumapili

Karibia watu 33 wamedhibitishwa kufariki nchini Kenya baada ya gari waliomokuwa wakisafiria kuanguka katika mto Nithi kwenye barabara kuu ya Meru-Nairobi siku ya Jumapili.

Ajali ya basi la kampuni ya Modern Coast nchini kenya iliyotokea katika kaunti ya Tharaka Nithi, 24 07 2022.
Ajali ya basi la kampuni ya Modern Coast nchini kenya iliyotokea katika kaunti ya Tharaka Nithi, 24 07 2022. © Daily Nation
Matangazo ya kibiashara

Kamishena wa polisi katika kaunti ya Tharaka Nithi eneo ambalo kumetokea ajali hiyo Nobert Komora amedhibitisha kuwa watu wengine 10 walinusurika katika ajali hiyo akionya kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kutokana na majaraha mabaya waliopata.

Polisi katika eneo hilo wanasema miili ya waliofariki inahifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti katika hosipatli ya rufa ya Chuka na hosipitali ya Chogoria inayomilikiwa na kanisa la PCEA.

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa 6.40 jioni Afrika mashariki baada ya basi hilo kuanguka katika mto huo uliofuta 40 chini ya daraja  ambalo ajali ilitokea.

Baadhi ya walioshuhudia ajali hiyo wanasema dereva alishindwa kulidhibiti basi hilo lilokuwa likiedeshwa kwa kasi kabla ya kuanguka kwenye mto huo.

Alex Mugambi afisa anayesimamia kitengo cha uwokozi katika kaunti ya Tharaka Nithi kwa ushirikiano na maofisa wa polisi na raia wameongoza shughuli za kuwatafuta manusura.

Eneo hilo ambalo kumetokea ajali hiyo limetajwa kama eneo hatari japokuwa madereva wamekuwa wakiendesha magari kwa kasi licha ya kutakiwa kupuguza kasi wanapokaribia kwenye daraja hilo.

Kutokana na kuongezeka kwa visa vya ajali zinazoripotiwa kutokea kwenye daraja hilo, raia wamekuwa wakitoa wito kwa mamlaka husika kutafuta suluhu swala ambalo halijatekelezwa.

Ajali nyengi zinazotokea kwenye daraja hilo zimehusishwa na kufeli kwa breki za gari.

Manusura wanaendelea kupokea matibabu katika hosipitali za hosipitali ya rufa ya Chuka na ile ya Chogoria inayomilikiwa na kanisa la PCEA.

Tayari tume inayosimamia usalama wa barabarani nchini Kenya,NTSA imesitsiha leseni ya kuhudumu kwa kampuni ya mabasi ya Modern coast ,kampuni inayomiliki basi hilo ambalo limehusika katika ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.