Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DR CONGO: Raia 29 wameuawa na waasi wa M23 tangu katikati ya mwezi Juni: HRW

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, linasema waasi wa M 23 wamewauwa raia 29 kuanzia katikati ya mwezi Juni, katika maeneo wanayadhibiti Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Raia wa Kivu kaskazini nchini Drc wakielekea mahali salama.
Raia wa Kivu kaskazini nchini Drc wakielekea mahali salama. UNHCR / P. Taggart
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii imeonesha miongoni mwa watu waliouawa ni vjana wawili waliotuhumiwa kutoa taarifa kwa jeshi la serikali FARDC kuhusu walikojificha waasi hao katika kijiji cha Ruvumu.

Aidha katika kijiji hicho, mama wa watoto watano mwenye umri wa miaka 35 katika ripoti hiyo amenukuliwa akisema baba yake alipigwa risasi kifuani huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma. 

Waasi hao wanaodaiwa kuungwa mkono na serikali ya Rwanda, pia walihusika na mauaji katika kijiji cha Ruseke, Julai mosi na wengine

Waliuawa katika kijiji cha Kabindi Kati ya Juni 23 na mwanzoni mwa Julai, ambapo Waasi hao walimuua mwanamume mwenye umri wa miaka 27 wakamvunja fuvu la kichwa kwa kutumia jembe dogo na kumng'oa macho yote mawili.

Ripoti hiyo pia imeenda mbali na kuonyesha kuwa Mwezi Mei na Juni, makombora yaliyorushwa na M23 kutoka upande wa mpaka wa Rwanda yaliharibu shule ya msingi, na kuua watoto 3 na mwanamke mmoja. 

Hata hivyo waasi wa M23 hawajatoa tamko lolote kuhusu ripoti hii na jitihada zetu za kuwatafuta hazijaza matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.