Pata taarifa kuu
Ukraine - Usalama

Ukraine : Urusi yashambulia bandari ya odesa

Makombora ya Urusi, yameshambulia bandari ya Odesa nchini Ukraine, siku moja baada ya nchi hizo mbili kusaini mkataba wa kuruhusu kusafirishwa kwa nafaka  kupitia habari nyeusi ili kupambana na uhaba wa chakula duniani.

eneo la  Odessa, kusini mwa Ukraine mnamo Julai 16, 2022.
eneo la Odessa, kusini mwa Ukraine mnamo Julai 16, 2022. © AP - Nina Lyashonok
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Ukraine wanasema makombora mawili kutoka kwenye jeshi la Urusi yamelega miundo mbiu ya bandari hiyo, huku kombora nyingine ikiangushwa na mitambo yake ya ulinzi.

Kitendo hiki cha Urusi kimelaaniwa na Mkuu wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell na kusema ni wazi Urusi haiheshimu makubaliano ya kimataifa na sheria.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress, amelaani pia hatua hiyo na kutaka Urusi kutekeleza kikamilifu mkataba wa kuruhusu usafirishwaji wa nafaka, kwa kuheshimu mkataba uliotiwa saini, baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na Umoja huo na nchi ya Uturuki.

Balozi wa Marekani nchini Ukraine Bridget Brink  naye ametaka Urusi kuajibushwa kutokana na kitendo hicho alichosema hakikubaliki na kuishtumu Moscow kwa kutumia chakula kama sillaha ya vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.