Guinea: Ujumbe wa ECOWAS kujadili kipindi cha mpito
Msuluhishi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, rais wa zamani wa Benin, Thomas Boni Yayi yupo jijini Conakry, kujadili mchakato wa kukabidhi madaraka kutoka kwa jeshi kwenda kwa uongozi wa kiraia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Msuluhishi huyo wa ECOWAS amepanga kukutana na viongozi wa kijeshi nchini humo, ili kujadiliana kuhusu muda unaokubaliwa wa kukabidhi madaraka kwa uongozi wa kiraia.
ECOWAS imetoa mpaka Agosti kwa uongozi huo wa mpito kuweka wazi mipango yake, la sivyo itawekewa vikwazo.
Msuluhishi huyo amekwenda jijini Conankry na pendekezo la kumtaka kiongozi wa Kijeshi Kanali Mamadi Doumbouya, kukubali mchakato wa miaka miwili utakaowezesha madaraka kurejea kwa raia, kwa kufanyika kwa uchaguzi.
Mbali na pendekezo hili, uongozi wa kijeshi pia unapendekeza kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya uongozi wa kijeshi na wanasiasa, lakini wanasiasa wakuu Sidya Touré na Cellou Dalein Diallo hawapo nchini.