Pata taarifa kuu
Ulaya - Mazingira

Ulaya : Nyuzi za juu za joto zahangaisha mataifa ya ulaya

Mataifa ya Ulaya Magharibi yanakumbwa na joto kubwa, ambalo sasa linaelezwa kuelekea katika mataifa ya Kaskazini

Moto ukiteketeza eneo la Landiras, huko Gironde, Julai 14, 2022.
Moto ukiteketeza eneo la Landiras, huko Gironde, Julai 14, 2022. © AP
Matangazo ya kibiashara

Joto linaelezwa kupanda hadi hasa nchini Ufaransa na Uingereza huku kiwango kikitarajiwa kufikia senti gredi 43 Kaskazini mwa nchi ya Uhispania, hivi leo.

Misitu katika nchi za Ufaransa,Ureno, Uhispania na Ugiriki inateketea na kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao.

Aidha, nchini Uingereza watalaam wanasema nchi hiyo inatarajiwa kushuhudia siku yenye joto kubwa, huku mji wa Nantes, Magharibi mwa Ufaransa ikirekodi kiwango cha joto cha sentigredi 42.

Watalaam wanasema ogezeko la joto linaloshuhudiwa barani Ulaya ni lkwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.