Pata taarifa kuu

Mkuu wa jeshi la Israeli kufanya ziara ya siku 3 nchini Morocco

Kiongozi wa jeshi la Israeli anatarajiwa kuanza zaira ya kikazi ya siku tatu nchini Morocco, hii ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa ngazi yake kwenye taifa hilo la Afrika kaskazini.

Benny Gantz, waziri wa ulinzi wa Morocco alipozuru Rabat mwezi Novemba.
Benny Gantz, waziri wa ulinzi wa Morocco alipozuru Rabat mwezi Novemba. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii imetajwa kuwa sehemu ya uhusiano mwema unaoedelea kati ya mataifa haya tangu Morocco kuungana na nchi zengine za uarabuni kurejesha uhusiano na Israeli Disemba 2020, harakati iliouungwa mkono pakubwa na utawala wa aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump. 

Tangu kurejeshwa kwa uhusiano huo , Maofisa wengine wa Israeli wamefanya ziara nchini Morocco, akiwemo waziri wa ulinzi wa Israeli Benny Gantz Novemba mwaka jana na baadae kufuatiwa na zaira yake waziri wa mambo ya  ndani Aylet Shaket mwezi Juni.

Israel na Morocco pia zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta za teknolojia, usalama, uchumi na masuala ya utamaduni.

Mwezi Machi, ujumbe wa wanajeshi kutoka Israeli ulifanya ziara ya kwanza nchini Morocco, ziara iliyopelekea kutiwa saini kwa makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi, pamoja na kuundwa kwa tume ya jeshi la pamoja.

Ziara hii inakuja siku chache baada ya rais wa Marekani Joe Biden kumaliza ziara yake nchini Israeli ambapo alielekea Saudia Arabia kwa kikao na viongozi wa mataifa ya Misiri,Jordan na Iraq.

Kikao hicho kiliangazia pakubwa taifa la Iran, uzalishaji wa mafuta, usalama wa chakula pamoja na ushirikiano na Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.