Pata taarifa kuu
AFIKA KUSINI - USALAMA.

Afrika Kusini: Watu 9 wameuawa kwa kupigwa risasi katika visa tofauti

Polisi nchini Africa Kusini, wanawasaka washukiwa waliowaua watu 9 kwa kuwapiga risasi katika visa viwili tofauti, usiku wa kuamikia Jumapili ya wikendi iliyopita.

Le président sud-africain Cyril Ramaphosa lors de son discours aux parlementaires, le 10 février 2022 à la mairie du Cap.
Le président sud-africain Cyril Ramaphosa lors de son discours aux parlementaires, le 10 février 2022 à la mairie du Cap. © AP/Nic Bothma
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya polisi imesema watu wanne walivamiwa katika mkoa wa Gauteng na watu wenye silaha ambapo waliwamiminia risasi na kuwaua wakati wa tukio hilo, wawili wakisalia na majiraha mabaya, kabla ya kuondoka.

Katika kisa kingine tofauti mwili wa mwanaume mmoja umepatikana katika jiji la Johannesburg ukiwa na majiraha ya risasi.

katika kisa cha tatu  polisi wanaendeleza uchunguzi katika mkoa wa Cape Magharibi kubaini waliohusika na vifo vya watu watatu wa familia moja, huku moja akiwa si wa familia hiyo, katika mji wa Khayelitsha.

Polisi wamesema hawafahamau sababu ya mauwaji hayo japo uchunguzi unaedelea.

Afrika Kusini kwa majumaa kadhaa sasa imekuwa ikishuhudia mauwaji yanayotekelezwa na watu wasiojulikana dhidi ya raia, watu 19 wakiuawa kwa risasi katika kipindi cha majumaa kadhaa yaliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.