Pata taarifa kuu
MALI- USALAMA

Wanajeshi 50 wa Ivory Coast wakamatwa nchini Mali.

Mamlaka nchini Mali inawazuia wanajeshi 50 raia wa Ivory Coast waliongia kwenye taifa hilo kufanya kazi kwa mwaliko wa kampuni iliyopewa kandarasi ya kikazi na ujumbe wa umoja wa mataifa nchini humo.

Wanajeshi wa Mali wakipiga doria katika eneo la Gao kaskazini mwa taifa hilo.
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria katika eneo la Gao kaskazini mwa taifa hilo. © AFP/Souleymane Ag Anara
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya serikali, imewataja wanajeshi hao wa Ivory Coast kama mamluki hatua ambayo inatajwa kuwa huenda ikazidisha uhasama kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika magharibi.

Msemaji wa serikali ya Mali, kanali Abdoulaye Maiga amesema ndege mbili ziliwasili katika uwanja wa ndege wa taifa lake siku ya jumapili zikiwa na wanajeshi 49 waliokuwa wamejihami kwa silaha na zana nyingine za kijeshi.

Mali imetaja uwepo wa wanajeshi hao katika ardhi yake kuwa kinyume cha sheria, na serikali ya mpito inawahusisha na makundi ya mamluki.

Msemaji wa ujumbe wa UN, Olivier Salgado, amekana  kuwa wanajeshi hao wa Ivory Coast ni sehemu ya walinda usalama wa MINUSMA , japokuwa wamekuwa nchini Mali kama njia moja ya kutoa huduma za usafiri kwa mojawapo ya kundi lao la walinda usalama.

UN, aidha imeeleza kuwa uwepo wa wanajeshi hao ulifaa kutambulishwa kwa mamlaka za Mali, wanajeshi hao wakitajwa na UN kuwa niwafanyakazi wa kampuni moja ya Ujerumani iliyopewa kandarasi na umoja huo kutoa usafiri wa anga kwa jina la Sahelian Aviation Services.

Msemaji wa serikali ya Mali akitaja kuwa watasitisha huduma za kampuni hiyo ya Sahelian Aviation Services inayomilikiwa na wanajeshi wa kigeni na kuwataka kuondoka katika ardhi yake.

Mwezi Juni serikali ya Mali ilitangaza kuwa haitakubali ujumbe wa UN kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu unaotekelezwa na wanajeshi wa Mali, hatua iliyosababisha Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.