Pata taarifa kuu
KENYA UGANDA- UCHUMI

Kenya Uganda: Wafanyabiashara walalamika kuhusu sheria za biashara kwenye ukanda.

Wiki moja baada ya sheria mpya kuhusu ushuru wa bidhaa kutoka nje ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki, kuanza kufanya kazi, tayari wafanyabiashara wameanza kulalama kuhusu sheria hiyo, wakitaka nchi wanachama kuifikiria upya sheria hiyo.

Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. fr.wikipedia.org
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Kenya na Uganda, zimewasilisha malalamiko kwa baraza la wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki, kuhusu sheria hiyo mpya iliyopandisha ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka nchi ambazo si wanachama wa Jumuiya hiyo hadi asilimia 35.

 

Mwezi mei, mawaziri wa Biashara na Fedha wa Jumuiya hiyo walipitisha asilimia 35 kama kiwango cha juu zaidi cha bidhaa zilizoainishwa chini ya sheria ya ushuru wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Kulingana na wataalamu, ushuru wa asilimia 35 kwa bidhaa zilizokamilishwa kutoka nje una uwezo wa kukuza biashara ya ndani kwa dola milioni 18.9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.