Pata taarifa kuu
Ghana - Afya

Ghana : Yaripoti visa vya virusi vya Marburg

Shirika la afya duniani (WHO) limesema watu wawili wamefariki nchini Ghana, kutokana na virusi hatari vya Marburg, ambavyo husabisha ugonjwa wa Ebola.

Taifa la Ghana kwa ramani ya Africa
Taifa la Ghana kwa ramani ya Africa © Google Map
Matangazo ya kibiashara

WHO inasema uchuguzi uliofanyiwa watu hao nchini Ghana umeonyesha walikuwa na virusi hivyo, lakini uchuguzi zaidi utafanyika nchini Senegal, kabla ya kuthibitisha rasmi iwapo iwapo walikuwa na virusi vya Marbur au la.

Taarifa ya WHO, imesema wagonjwa wawili kutoka eneo la Ashanti walikuwa na maumivu ya kutapika na kuumwa na kichwa pamoja na kuendesha na baadaye wakafariki.

Iwapo visa hivi vitathibitishwa basi utakuwa mlipuko wa pili kuripotiwa Africa magharibi, baada ya kutokea kwa mlipuko mwingine mwaka uliopita nchini Guinea, WHO ikisema tayari imejiandaa iwapo patatokea mlipuko wa virusi hivyo.

Pamekuwa na visa vya virusi hivyo barani Africa tangu mwaka 1967, vingi vikiripotiwa kusini mwa Africa na Africa mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.