Pata taarifa kuu
Angola - Kifo

Angola : Rais wa zamani Dos Santos  afariki

Rais wa zamani wa Angola, José Eduardo dos Santos, aliyeongoza Angola kwa zaidi ya miaka 40, amefariki akiwa na umri wa miaka 79, serikali ya taifa hilo imetangaza.

Rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos
Rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos AFP PHOTO/ JOAO CORTESAO
Matangazo ya kibiashara

Dos santos amefiri akiwa nchini Hispania ambako amekuwa akipokea matibabu kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi.

Dos Santos atakumbukwa pakubwa kwa kuchangia kumalizika kwa vita nchini Angola, mapema miaka ya 2000, huku akifahamika baba wa Amani.

Hata hivyo utawala wake ulihusishwa pakubwa na rushwa na ukiukaji wa haki za binadamu.

Dos Santos mhandisi katika sekta ya mafuta kutoka muungano wa Kisoviet mwaka 1969, aliingia madarakani akiwa na miaka 37, baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Angola, António Agostinho Neto.

Miaka 4 baada ya Angola kupata uhuru  taifa hilo lilizama kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, kati ya pande mbili pinzani ambayo zilikuwa zimepambana na utawala wa kikoloni, Chama cha Dos Santos MPLA na Unita.

Vita hivyo vilidumu kwa miaka 27, zaidi ya raia 500, 000 wakiripotiwa kufariki.

Vita hivyo vilichangia taifa la Cuba kuwatuma wanajeshi wake nchini Angola kushika doria kwa niaba ya serikali huku Africa Kusini ikiwatuma wanajeshi wake nchini humo kupigania maslahi ya Unita chini ya kiongozi wake  Jonas Savimbi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.