Libya : Beltress laitisha maandamano Zaidi
Maandamano zaidi yanazidi kushuhudiwa nchini Libya, raia wakilalamikia kupanda kwa bei ya vyakula, ukosefu wa nguvu za umeme na mzozo wa kisiasa nchini humo.
Imechapishwa:
Vijana wenye hasira wameonekana wakiwasha magurudumu ya magari na kufunga barabara zikiwemo barabara kuu jijini Tripoli, Polisi wakikosa kuingia kati kutuliza hali .
Maandamano hayo yanaongozwa na vuguvugu kwa jina Beltress, ambalo linasema linapanga maandamano zaidi, kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi na kuvunjwa kwa mabunge yote mawili ambayo yanahasimiana.
Mwishoni mwa juma lililopita wandanaji hao walivamia bunge la mashariki eneo la Tobruk, na kuteketeza sehemu ya jengo la bunge hilo
Taifa la Libya limekuwa kwenye mzozo tangu mwaka 2011, wakati kiongozi wa taifa hilo Moamer Kadhafi, aliondolewa madarakani na kuuawa.